1. Utangulizi
Karibu CHIMBO PLATFORM. Kwa kujiunga na jukwaa letu, unakubali sheria na masharti yote yaliyoorodheshwa hapa chini.
2. Masharti ya Kujiunga
- Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi.
- Taarifa zote unazotoa lazima ziwe sahihi na za kweli.
- Hautaruhusiwa kutumia jukwaa kwa shughuli zisizo halali.
3. Wajibu wa Mtumiaji
- Kutunza usiri wa neno lako la siri.
- Kutoa taarifa sahihi wakati wa usajili.
- Kufuata sheria zote za nchi yetu Tanzania.
4. Uthibitisho wa Taarifa
CHIMBO ina haki ya kuthibitisha taarifa zote zilizotolewa.
5. Faragha ya Taarifa
Taarifa zako za kibinafsi zitalindwa na kutumika kwa madhumuni ya jukwaa tu.